Jump to content

Fundraising 2012/Translation/Sengai appeal

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Fundraising 2012/Translation/Sengai appeal and the translation is 100% complete.
  • Tafadhali soma:
    Rufaa binafsi kutoka kwa
    Mwandishi wa Wikipedia Dr. Sengai Podhuvan

Appeal

Kutoka kwa mwandishi wa Wikipedia Dr. Sengai Podhuvan

Nilizaliwa mkulima maskini katika maeneo ya vijijini India mwaka wa 1936. Leo nategemea na kuhariri Wikipedia.

Nataka Wikipedia iwe hapa kwa ajili ya vizazi vyote vijavyo. Hii ni shughuli yetu ya kutafuta fedha ya kila mwaka ili tuilipe seva zetu, wafanyakazi wetu wadogo na miundombinu mingine ambayo inafanya Wikipedia iendelee kwenye mtandao kwa bure na bila ya matangazo. Kama unaweza, tafadhali fikiria kuchanga $5, $20, $50 au chochote unachoweza.

Baada ya kupata umri kama wangu, ungetaka kushiriki ujuzi na uzoefu pamoja na ulimwengu. Juu ya kozi ya maisha yangu, aniikuwa mwalimu, nikachuma PhD, nilikuwa mhariri wa gazeti la serikali kwa miaka 14, nikakuwa baba ya binti watano na mtoto mmoja wa kiume na bado najifikiria kama mkulima wa nchi na jembe moja.

Niliandika PhD yangu juu ya mada ya michezo ya jadi katika Jimbo la India la Tamil Nadu. Labda kamwe hauta angalia moja ya makala yangu. Lakini inaniridhisha mimi kwamba maelfu wanaziangalia. Na mimi nina fahari ya kuwa kila somo unalotaka kujifunza, kuna uwezekano wa kulipata kwa Wikipedia.

Wakati mimi niliponunua kompyuta yangu ya kwanza mwaka 2005, kwa kutumia puku tu ilikuwa vigumu kwa sababu mikono yangu hutetereka. Lakini manmo 2009 nilikuwa nimegundua Wikipedia. Siku moja, mimi niliumba makala kuhusu washairi wa kale wa kihindi. Niliongeza takriban majina 30 yao kwa ukurasa na kisha nikaenda kulala. Asubuhi, nilipata majina 473 juu ya ukurasa huo. Hiyo ndiyo inafanya Wikipedia!

Tafadhali fikiri kujiunga na juhudi zetu kwa kuhariri au kwa kufanya mchango kuweka Wikipedia bure.

Asante,

Dr. Sengai Podhuvan PhD
Mwandishi wa Wikipedia