Movement Strategy/Recommendations/Summary/sw
Safari ya Mkakati wa Mradi inahusu watu. Watu wanaochangia na kutumia maarifa na watu wanaojumuisha jamii na makundi mbalimbali ambao ni msingi wa Mradi wetu. Mwaka 2017, tulianza safari ya kutengeneza siku za usoni za Mradi wetu. Tulijiwekea Mwelekeo wa Kimkakati wa mambo makuu: kuwa muundombinu muhimu wa mfumo wa ikolojia ya maarifa bila malipo kufikia mwaka wa 2030. Kuhakikisha kwamba mtu yeyote anayeshiriki katika maono yetu ataweza kujiunga nasi, tunajitahidia usawa wa maarifa na maarifa kama huduma.
Katika kipindi cha miaka miwili, watu kutoka kote kwenye Mradi walishirikiana katika mchakato wa mkakati wazi na wa ushiriki ili kujadili jinsi ya kuimarisha mifumo yetu ili kutuwezesha kufanikisha Mwelekeo wa Kimkakati. Hati hii inawasilisha matokeo ya juhudi hizi za pamoja: mapendekezo 10 na kanuni 10 zinazoobainisha mwongozo wa mabadiliko. Baadhi ya dhana zina msingi kwenye mafanikio yaliyopo na ustadi na uzoefu mkubwa uliopo kwenye Mradi wetu na hata zaidi. Wengine wanataka kuona mabadiliko kwenye jinsi tunavyoendesha, kutangamana, na kutetea misheni na maadili yetu. Na wengine wanatuhitaji kubuni njia mpya za kufanya kazi, kushirikiana, na kutawala ili kuweza kupata mafanikio endelevu ya Mradi wetu.
Hii kazi imefanywa na Wanawikimedia karibu 100 kutoka kote ulimwenguni, ikijumuisha, wajitoleaji, wafantikazi na memba wa bodi za washirika na Asasi ya Wikimedia, na wawakilishi kutoka kwa mashirika marafiki. Walijikusanya katika makundi tisa, kila kundi likifanya utafiti, majadiliano, na kuandika rasimu za dhana katika mikutano ya mtandaoni na ya ana kwa ana. Watu wengine wengi binafsi walishiriki maoni, kuchangia katika majadiliano, na kuchangia mtandaoni na katika matukio mengi. Mapendekezo ya sasa ni tokeo la marudio rudio manne makuu kuanzia mwezi Agosti 2019. Kulingana na maoni na ushirikiano, makundi hayo yalitayarisha marudio ya pili mwezi Septemba yalijumuisha mapendekezo 89. Mapendekezo haya yalijumuishwa na waandishi binafsi katika kundi la mapendekezo 13. Maoni mazuri yaliyopokewa kuanzia Januari hadi Machi 2020 yalisaidia kuimarisha mapendekezo na kuyatamatisha na kuwa yalivyo hizi sasa: mapendekezo kumi na kanuni kumi.
Principles
Kanuni hizi ni maadili msingi kote katika Mradi kwa ambayo mapendekezo yamebuniwa na yatatekelezwa. Kanuni hizi ni: kuangazia watu, usalama na ulinzi; ujumuishaji na ufanyi maamuzi kwa mashirikiano; usawa na uwezeshaji; uwekaji matawi na kujitawala; uwekaji katika muktadha; ushirikiano; uwazi na uwajibikaji; ufanisi; na uvumilivu. Kanuni hizi zinazohusiana kwa karibu zinazungumzia kile ambacho Mradi wetu unahitaji kufanya ili kuwa muundombinu muhimu wa mfumo wa ikolojia ya maarifa bila malipo.
Recommendations
Yakiwa na kanuni hizi katika kiini chake, mapendekezo 10 ya Mkakati wa Mradi yanawasilisha mabadiliko yanayotegemeana kwa karibu ambayo yanaleta nafasi ya siku za usoni za Mradi wa Wikimedia:
Kuongeza Uwezo wa Mradi Wetu Kujitegemea pendekezo hili linatuhimiza kuwaangazia watu na kuwekeza katika mahitaji ya watu. Uwezo wa Mradi wetu kujitegemea unategemea kutambua na kuunga mkono uanuwai wa wachangiaji wetu - wajitoleaji waliokita mizizi na wageni - na shughuli zetu. Pendekezo hili linaangazia njia za usawa za kusambaza ufadhili na fursa mpya kwa ajili ya kuzalisha mapato, kuongeza uhamasisho kuhusu Mradi, kukuza uwezo wa uchangishaji fedha katika maeneo yetu, na kukuza ubia wenye uanuwai.
Kuimarisha Huduma ya Mtumiaji pendekezo hili linaangazia urahisi wa bidhaa zetu kutumika na kufikika na njia endelevu za kuziimarisha. Linapendekeza kuwahusisha wachangiaji na jamii za watengenezaji katika utafiti, muundo, na ufanyaji majaribio wa profaili na vifaa mbalimbali. Pia linajumuisha rasilimali za wageni, viwando vya rekodi, zana za baina ya miradi na baina ya lugha, kuimarisha miradi, na utengenezaji API.
Utengenzaji Sheria za Kinidhamu, kuripoti tukio bila kujitambulisha, na kuanganzia unyanyasaji katika miradi yetu zimejadiliwa katika Uzingatiaji Usalama na Ujumuishaji. Pendekezo hili linapendekeza msingi wa tabia inayokubalika katika Mradi, mpango wa kutathmini usalama na utekelezaji ambao unajumuisha muundombinu wa ukabilianaji kwa haraka, kukuza uwezo wa ndani wa usalama na ulinzi, utetezi wa mifumo ya kisheria ambayo ni mizuri kwa mradi wa maarifa bila malipo, na zana za usiri zilizobinafsishwa kulingana na eneo ili kuhakikisha usalama wa wachangiaji.
Kuhakikisha Usawa katika Ufanyaji Maamuzi pendekezo hili ni msingi katika kuweka jukumu la wajibu wa pamoja katika Mradi. Uwakilishi wa usawa katika ufanyaji maamuzi kwa njia wazi, uwezeshaji jamii wenyeji, na upeanaji rasilimali za ushirikiano zote ni mada muhimu katika pendekezo hili. Linapendekeza Kitengo Maalum cha Mradi, uwekaji wa Baraza la Kiulimwengu, vituo vya kimaeneo na kimuktadha, na majukumu yaliyobainishwa wazi, na miongozo ya ushiriki kwa washikadau wote.
Kuendeleza kwenye majukumu na wajibu uliobainishwa wazi, Kuratibu kwa Washikadau pendekezo hili linapendekeza kutengeneza nafasi ya mawasiliano na ushirikiano ulioimarishwa ndani ya Mradi na pamoja na wabia, wachangiaji wa kiufundi, na jamii za watengenezaji kwa ajili ya uratibu wa teknolojia. Linapendekeza kuratibu rasilimali, kuweka Baraza la Teknolojia kwa ajili ya utendaji mpya, ubadilishaji maelezo kwa kina, mafunzo yaliyoimarishwa na uhamishaji maarifa, na fursa za mtandao.
Kuwekeza katika Uimarishaji Ujuzi na Uongozi pendekezo hili linaangazia kuimarisha ujuzi wa kiufundi na wa watu kwa njia ya usawa katika watu na mashirika katika Mradi wetu. Hii inahitaji mkabala wa kiulimwengu kwa utaratibu pamoja na miradi husiani ya wenyeji kwa ajili ya ujuzi mbalimbali. Mikabala itawekwa katika muktadha na kujumuisha mafunzo mtandaoni, mitandao ya kirafiki, utengenezaji maudhui kwa lugha nyingi, mashauriano, na utambuaji na fidia za ukuzaji ujuzi. Pendekezo hili linapendekeza mpango wa pamoja wa ukuzaji uongozi kwa watu binafsi na muundombinu hitajika (mtandaoni na nje ya mtandao) ili kuwezesha uhamishaji maarifa.
Kudhibiti Maarifa ya Ndani pendekezo hili linapendekeza kuhakikisha kwamba maarifa ya ndani ya Mradi ni rahisi kutumika, ni ya ushirikiano, na ya ubora wa juu. Kulingana na pendekezo hili, tunahitaji utamaduni wa kuweka rekodi, msingi wa maarifa ulio na nyenzo za mafunzo, na usaidizi kutoka kwa wafanyikazi waliopatiwa jukumu hili.
Kuheshimu uhuru wa wajitoleaji, Kutambua Mada zenye Athari Kubwa pendekezo hili linatuomba kuelewa jinsi maudhui yetu yanavyoathiri watu na linatupatia njia za kuangazia pengo kwenye maudhui, kuelewa madhara makubwa ya kutoa maelezo yasiyo sahihi kuhusu miradi yetu, kutetea na kuweka kipaumbele rasilimali zinazohusiana na utengenezaji maudhui, na kushirikiana na wabia wa taaluma mahsusi.
Kuwa Wabunifu katika Maarifa Bila Malipo pendekezo hili linatuomba kukagua na kupanua miradi yetu mbalimbali na umbizo mbalimbali za maudhui ili kusalia kuwa muhimu na kutoa ufikiaji kwenye maarifa yote ya wanadamu. Pendekezo hili linapendekeza kutambua, kwa kushirikiana na jamii, sera na mazoea ambayo ni vizuizi vya usawa wa maarifa, vya utengenezaji njia za miradi mipya, na vya utengenezaji zana na ubia wa kufanya maarifa bila malipo kufikiwa kwa umbizo na mifumo mbalimbali ya matumizi.
Ili kuweza kutekeleza mkakati wa Mradi kwa ufanisi, tunahitaji kukuza uhamamisho wa watu binafsi na mashirika na Kukagua, Kurudia Rudia, na Kutumia kazi zetu. Hii inahitaji rasilimali, ustadi na uwezo, jukumu la pamoja, na wajibu wa pamoja wa kukagua, kuwasilisha maendeleo, kuwezesha mafunzo, na kutumia kazi zetu.
Utekelezaji wa mapendekezo haya kumi na kanuni husika kutapelekea mabadiliko msingi ya kitamaduni na kimfumo ambayo yatawezesha Mradi wetu kuwakaribisha wote wanaoshiriki maoni yetu ya ‘ulimwengu ambapo kila mwanadamu anaweza kushiriki kwa uhuru katika maarifa yote kwa ujumla.’ Kwa kutekeleza mabadiliko haya kwa ushirikiano katika miaka ijayo, tutahitaji kuweza kuangazia mahitaji ya watu wote ambao ni msingi wa Mradi wetu na wale wanahudumu - sasa hivi na katika siku zijazo - na kuwa muundombinu muhimu wa mfumo wa ikolojia ya maarifa bila malipo.