Jump to content

Mkataba wa Harakati/Kamati ya Kuandika/Tangazo - Kura ya Uidhinishaji inafunguliwa

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Movement Charter/Drafting Committee/Announcement - Ratification vote opens and the translation is 100% complete.

Upigaji kura ili kuidhinisha Mkataba wa Harakati wa Wikimedia sasa umefunguliwa - piga kura yako

Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki. Please help translate to your language

Habarini nyote,

Upigaji kura wa kuidhinisha Mkataba wa Harakati za Wikimedia sasa umefunguliwa. Mkataba wa Harakati wa Wikimedia ni hati ya kufafanua majukumu na wajibu kwa wanachama na vyombo vyote vya harakati za Wikimedia, ikijumuisha kuundwa kwa chombo kipya - Baraza la Kimataifa - kwa ajili ya utawala wa harakati.

Toleo la mwisho la Mkataba wa Harakati za Wikimedialinapatikana kwenye Meta katika lugha tofauti.

Upigaji kura ulianza kwenye SecurePoll mnamo Juni 25, 2024 saa 00:01 UTC na utakamilika mnamo Julai 9, 2024 saa 23:59 UTC. Tafadhali soma zaidi kuhusu maelezo ya mpigakura na maelezo ya ustahiki.

Baada ya kusoma Mkataba, tafadhali piga kura hapa na ushirikishe dokezo hili zaidi.

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu kura ya uidhinishaji, tafadhali wasiliana na Tume ya Uchaguzi ya Mkataba kwa cec@wikimedia.org.

Kwa niaba ya CEC,