Maangazo ya Wikimedia, Aprili 2012
Maangazo kutoka kwa Ripoti ya Wakfa wa Wikimedia na Ripoti ya Uhasibu wa Wikimedia ya Aprili 2012, na chaguo za matukio mengine ya maana kutoka kwa harakati za Wikimedia
Maangazo ya Wakfa wa Wikimedia
Kupanua miundo ya kuchangisha fedha na miundo ya uhusiano
Baada ya maazimio ya Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia katika mkutano wake Berlin, kazi inaendelea kutekeleza muundo mpya wa kusambaza pesa zinazochangishwa kupitia tovuti za miradi ya Wikimedia. Isipokuwa gharama kwa ajili ya shughuli za msingi na hifadhi ya uendeshaji wa shughuli za WMF, yote (ikiwa ni pamoja na fedha kwa ajili ya sura na shughuli zisizo za msingi za WMF) zitagawanywa kwa kuzingatia mapendekezo ya Funds Dissemination Committee (FDC) inayoendeshwa na wahanga. Azimio lingine bodi inatambua mifano mipya ya uhusiano na harakati ya Wikimedia: "Washirika wa Harakati" (mashirika yenye madhumuni sawa ambayo yanasaidia kazi ya harakati), "Sura za Kitaifa na za kiji taifa" (amabyao inajumuisha muundo wa sasa wa sura) "Mashirika Thematic" (yasiyo ya faida yanayowakilisha harakati na kutumia alama za biashara za Wikimedia, ambayo ni kusaidia kazi iliyolenga mada, maalum), na "Vikundi vya Watumizi" (makundi ya uanachama wazi wanaweza au kukataa kuchagua kuingiza)
Kuwafikia Lugha za asilia ya Kihindi
Afisa Mkuu wa Maendeleo ya dunia nzima, Barry Newstead alitembelea India akikutana na wana Wikimedia wa Bangalore na akahudhuria Wikisangamotsavam, mkutano wa jamii ya Malayalam, kama sehemu ya kazi ya kusaidia miradi lugha zenye asili ya Kihindi. Timu ya India inafanya kazi kikamilifu na jamii saba za Kihindi juu ya mikakati ya kuwafikia, mikakati ya vyombo vya habari vya kijamii na mipango ya kujenga jamii kasi.
Lengo la kurasa zilizoonwa kwa simu kufikiwa
Mwishoni wa Aprili, tovuti ya Wikipedia ya simu ya mkono ilifikia hatua ya kurasa bilioni 2 kila mwezi zinazoo onwa - moja ya malengo ya mpango wa 2011/12 wa WMF wa mwaka.
Kulekea kwa mzunguko wa kutekeleza programu kwa haraka
Wahandisi wa Wikimedia wameanza Kubadilisha kwa mzunguko wa haraka, kuanza kutimiza programu ya hivi karibuni ya Mediawiki kwa Wikipedia na tovuti zingine za Wikimedia kila wiki mbili.
Takwimu na Mwelekeo
Wageni wa kipekee wa Machi:
- Milioni 489 (+ 2.7% ikilinganishwa na Februari, +22.3% ikilinganishwa na mwaka uliopita)
- (takwimu ya comScore kwa za miradi yote ya Wakfu wa Wikimedia; comScore itatoa takwimu za Aprili baadaye mnamo Mei)
Maombi ya Kurasa ya Aprili:
- bilioni 17.3 (+0.4% ikilinganishwa na Machi; +18.2% ikilinganishwa na mwaka uliopita)
- (logi ya takwimu ya seva, Miradi yote ya Wikimedia ikijumuisha na wanaopata kwa njia ya simu)
Wahariri waliosajiriwa wa Machi 2012 (>=5 hariri/mwezi)
- 85.09K (+0.2% ikilinganishwa na Februari / -4.5 ikilinganishwa na mwaka uliopita)
- (Takwimu za hifadhidata, miradi yote ya wakfu wa Wikimedia isipokuwa Wikimedia Commons)
Ripoti Kadi ya Machi 2012: http://reportcard.wmflabs.org/
Fedha
(Taarifa za fedha inapatikana tu ya mwezi Machi 2012 wakati wa taarifa hii.)
Taarifa zote za fedha zilizowasilishwa ni kwa kipindi cha Julai 1, 2011 - Machi 31, 2012.
Mapato | $ 32,054,861 |
---|---|
Matumizi: | |
Kikundi cha Teknolojia | $ 7,788,192 |
Jamii/Kikundi cha Kuchangisha Fedha | $ 3,212,763 |
Kikundi cha Ukuaji Duniani kote | $ 2,984,100 |
Kikundi cha Utawala | $ 718,116 |
Fedha/Kisheria/Raslimali Watu/Kikundi cha Usimamizi | $ 4,607,656 |
Jumla ya Matumizi | $ 19,310,826 |
Jumla ya mabaki/(hasara) | $ 12,744,035 |
- Mapato ya mwezi ni $ 1.9MM ikilinganishwa na mpango $ 3.9 MM, kwa kukadiria $ 2 MM ama 53% chini ya mpango.
- Mwaka-hadi-sasa ni $ 32.1 MM ikilinganishwa na mpango $ 28.6 MM, ikikadiriwa ni $ 3.5 MM ama 12% juu ya mpango.
- Matumizi ya mwezi ni $ 2.3MM ikilinganishwa na mpango wa $ 2.2MM, kwa kukadiria ni $ 112K ama 5% zaidi ya mpango.
- Mwaka kufikia sasa ni $ 19.3MM ikilinganishwa na mpango $ 21.1MM, ikikadiriwa $ 1.8MM ama 8% chini ya mpango.
- Nafasi ya fedha ni $ 30.6MM mnamo Machi 31, 2012 - ikikadiriwa ni miezi 13 ya matumizi.
Maelezo mengine ya Harakati
"Mwana Wikipedia katika makazi" muundo wake umekomaa
Maktaba ya Uingereza ndiyo taasisi ya kitamaduni ambayo hivi karibuni kutangaza (pamoja na Wikimedia UK) mwana Wikipedia wa makazi, akisaidia uhusiano kati ya wafanyakazi wa Maktaba ya Uingereza na jumuiya ya Wikimedia . Katika mkutano wa kifahari wa Wanachama wa Marekani 2012, wana Wikipedia watano wa makazi kutoka duniani kote walionyesha muundo huo wa ushirikiano. Toleo la Aprili la "Huu mwezi katika GLAM" na barua ya taarifa ina ripoti nafasi zilizo wazi za Wana wikipedia wa makazi katika taasisi za kiserikali huko Israeli, Ujerumani na Uswidi.
Wikidata yaanza kufanya kazi kwa viungo vya wiki hadi wiki
Katika mwezi wake wa kwanza,timu ya Wikidata imeanza kuandiaka programu katika awamu ya kwanza ya mradi huu, ambayo itaruhusu kuhifadhi kwa pamoja kwa viungo vya wiki hadi wiki. Matawi mawili ya Mediawiki yanatengenezwa kama ngome ya Wikidata:koteja ya Wikibase na msingi wa Wikibase.Toleo la kuonyehsa litapatikana hivi karibuni.
Mashindano ya lugha tofauti kutoka kwa mradi wa Monmouthpedia
Kama sehemu ya Monmouthpedia - "mradi wa kwanza wa Wikipedia utakaofanywa kwenye mji mzima" - Charles Rolls Challenge ni zawadi ambazo zitatuzwa wana wikimedia ambao walikuwa wameandika, kuboresha ama kupakia maudhui kuhusu Monmouth katika lugha tofauti. Pia, mji huo uliona mkutano wa kwanza kabisa wa Kiwelisi mnamo Aprili.
Mashindano ya filamuna picha ya Tamil
Jamii ya Wikimedia ya Tamil [1] Mashindano yake ya filamu na picha ya Wiki ya Tamil", ambayo ilitokea kwa michango 15,000 ya picha na video kutoka kwa watu 307.
Kampuni ya hifadhidata yapea Wana Wikimedia fikio la bure
Zaidi ya wana Wikimedia 600 wamepokea fikio ya bure kwa hifadhidata ya Utafiti wa Highbeam kwa mwaka mmoja, ili kuendeleza kazi yao kwa Wikipedia na miradi mingine dada zake. Wahariri wa kawida wanaweza bado wakaweka ombi kupitia Ukurasa wa maombi wa mradi.