Kamati ya Masuala ya Jamii ya Wikimedia Foundation/Mazungumzo: 2024
Karibu kwenye Mazungumzo: 2024, mazungumzo ya kushirikisha, kusikiliza, na kujifunza tukiwa na dhamira kadri tunavyoendelea kupanga mustakabali wetu kama harakati. Ili kuongelea kuhusu Kuzungumza, angalia Majadiliano.Taarifa zaidi hapa chini.
Mkurugenzi Mtendaji(CEO) Maryana Iskander wa shirika la Wikimedia Foundation hivi karibuni alishirikisha ujumbe huu akitafakari kuhusu maendeleo tangu ziara yake ya kwanza ya kusikiliza mwaka wa 2021 iliyolenga kuelewa changamoto na mahitaji yanayozikabili harakati za Wikimedia.
Miaka miwili baadaye, mengi yamebadilika ulimwenguni na katika jamii zetu. Mfululizo huu wa mazungumzo unakusudiwa kuweka juhudi zaidi na makusudi katika kuwasilisha taarifa sahihi, kwa wakati ufaao, na kwa njia ifaayo, hata kama tunajua kwamba hatuwezi kamwe kukidhi matarajio ya kila mtu. Pia ni muhimu kuzungumza baina yetu kwa mwaka mzima - kwa njia rasmi na za kawaida.
Katika kipindi cha miezi michache ijayo, Kamati ya Masuala ya Jamii, viongozi wakuu katika Shirika, na Maryana watapatikana ili kuuliza: una mawazo gani kuhusu matukio muhimu yatakayotokea mwaka wa 2024, kuhusu mpango wa kila mwaka wa Shirika, au vipaumbele vyetu vya muda marefu?
Tuzungumze
Natumai utaamua kushiriki. Unaweza kuchangua kujiandikisha kushiriki kwenye wiki na nje ya wiki, ikiwa ni pamoja na mazungumzo binafsi na Wadhamini, na mimi mwenyewe au na viongozi wengine wa Shirika.
— Maryana Iskander, Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Shirika la Wikimedia Foundation
Ili kushiriki katika Mazungumzo: 2024, tafadhali bofya "jisajili hapa", jaza fomu, na uhakikishe kuwa umeangalia ukurasa wako wa majadiliano au uwashe kipengele cha "tuma barua pepe kwa mtumiaji huyu". Mhusika kutoka kwenye timu ya Mawasiliano ya Harakati atawasiliana nawe.
Unaweza pia kututumia barua pepe kwa movementcommswikimediaorg. Tafadhali tujulishe ikiwa ungependa kikao binafsi cha mtandaoni au kama kuna wengine ambao ungependa wajiunge nawe kwenye mazungumzo. Je, kuna mtu mahususi ungependa kuzungumza naye? Je, unapendelea kuzungumza kwa Kiingereza au tunaweza kukusaidia kwa ukalimani wa moja kwa moja? Na Pia, upatikanaji wako. Tutajaribu tuwezavyo ili kuoanisha.
Tunatazamia kuzungumza nawe.
Oktoba 2023 Sasisho na mwaliko wa Mazungumzo: 2024
Habarini nyote,
Tangu nijiunge na Wikimedia Foundation, nimejaribu mara kwa mara kuwatumia masasisho hapa na penginepo. Ninakumbuka kuwa hii inafika wakati wa kipindi cha changamoto mtambuka kote ulimwenguni huku vita vinavyoongezeka, mizozo, na hali ya hewa vikitukumbusha kila wiki kuwa hali tete ya kidunia na kutokuwa na uhakika wa mambo yajayo kunaongezeka. Natumai utasoma ujumbe huu hadi mwisho ili kuungana nami na uongozi wa Shirika katika mazungumzo kati yetu wakati ninapohisi tunahitaji kukaribiana zaidi.
Jinsi mambo yalivyoanza...
Miaka miwili iliyopita mwezi kama huu, nilianza mchakato wa kusikiliza na kujifunza kujiandaa kwa ajili ya kuanza kwangu rasmi kwenye Shirika. Katika mazungumzo ya kibinafsi na karibu watu 300 kutoka nchi 55, pamoja na matukio mengi ya jumuiya, niliuliza maswali kuhusu maono na dhamira ya Wikimedia, kile tulichoamini ulimwengu unahitaji kutoka kwetu kwa sasa, na changamoto gani tulizokabiliana nazo katika kufikia malengo yetu. Hii ilipelekea kuwa na ‘mafumbo’ matano ambayo naamini yanaendelea kutusumbua.
Niliona wakati huo kwamba mada pekee yenye makubaliano ya pamoja ilikuwa hitaji la dharura la kazi yetu - ambalo ni kweli linahitajika sasa kuliko hapo awali. Kadiri habari potofu/upotoshaji unavyoongezeka, huku mgawanyiko na migogoro ikiongezeka katika jamii kote ulimwenguni, miradi ya Wikimedia inasalia kujitolea kwa kanuni za maarifa ya wazi na kutoegemea upande wowote. Hakuna shaka juu ya umuhimu na uhitaji wa uharaka wa michango yetu.
Ulimwengu unahitaji sisi kufanikiwa, na hilo linanifanya nione vizuri zaidi katika ulimwengu tunaoishi leo. Wakati baadhi ya maeneo ya jamii yetu yanatilia maanani juu ya kinachotokea karibu nasi, naamini bado hatujaungana vya kutosha dhidi ya vitisho hivi na vitisho vingine vinavyotukumba sote
Mazungumzo yangu ya mwaka 2021 yalichangiwa na kile ambacho wajitoleaji walifikiri kuhusu jinsi ya kufanya michango yote kuthaminiwa, jinsi ya kufanya hali yetu ya kuwa na lugha nyingi kuwa yenye nguvu zaidi, na jinsi ya kuvunja fumbo la duara la kusimamia taasisi za serikali kuu kusaidia miradi iliyogatuliwa. Nilithamini sana maoni kuhusu jinsi ya kuziba pengo la kati ya tulipo na tunapohitaji kuwa katika kujenga miundombinu ambayo inaongozwa na binadamu, na inayowezeshwa kwa nguvu na teknolojia.
Mambo yanavyoendelea...
Tangu wakati huo, nimekuwa nikitilia mkazo hasa utendaji na uwajibikaji wa Shirika la Wikimedia Foundation - pengine kwenu nyote, lakini pia kwa wasomaji wetu, wafadhili, wadhibiti na washirika wetu. Tathmini yangu binafsi mwanzoni mwa 2023 ilikuwa kwamba tulikuwa tukielekea zaidi katika mwelekeo sahihi: mpango wa mwaka wa Shirika unaongozwa na mkakati wa harakati na kujaribu kuwa na mwitikio zaidi kwa mahitaji ya watu wanaojitolea, tuna zaidi ya mara tatu ya idadi ya lugha tunazowasiliana nazo kwenye maeneo mbalimbali kote ulimwenguni, na tume pangilia upya vipaumbele vya teknolojia ili kusaidia vyema mfumo wa maarifa unaobadilika haraka.
Malengo ya kila mwaka yanapaswa kufafanuliwa kwa uwazi, na kisha kutekelezwa vizuri. Lakini kazi yetu inahitaji muda mrefu zaidi kuliko upangaji wa kila mwaka - hakika hadi 2030, ambayo naamini inahitaji kuuliza maswali magumu zaidi kuhusu vipaumbele, vikwazo, na mabadiliko ya biashara ili kukubaliana kivitendo juu ya kile kinachoweza kupatikana katika miaka saba ijayo na ukuaji wa polepole wa rasilimali na miundo yetu ya sasa ya ushirikiano.
Swali la uwanda wa wakati pia linaongoza kwa kuulizwa kama Wikipedia itakuwa kitu muhimu kwa kizazi kimoja au kama tunajua jinsi ya kuendeleza Wikimedia kwaajili ya vizazi vijavyo. Dhamira yetu inataka kazi hii iendelee kudumu, na baadhi ya vipengele vya miradi yetu vimeunda alama za kidijitali duniani ambazo huhisi kuwa haziwezi kufutika. Lakini mtazamo wa vizazi vingi wa Wikimedia unahitaji nini kutoka kwetu, kuanzia sasa? Ninaamini kuwa hili halihusu kauli za hali ya juu kuliko kufanya kazi kwa nia ya makusudi katika masuala ambayo yatasaidia kuleta mtazamo wa vizazi vingi wa miradi yetu katika mwelekeo ulio wazi zaidi, sasa na hapo baadaye.
Baadhi(si yote) ya maswali makubwa...
Sina hakika jinsi ambavyo tunapaswa kulitimiza hili, na ninatumai kusikia unachofikiria (zaidi kuhusu hili angalia hapa chini). Kwa sasa, nimeomba uongozi wetu wa Bodi ya Wadhamini na Shirika kuweka malengo ya Mpango wa miaka mingi na mada tatu ambazo zinahisiwa kuwa ni mahali pazuri pa kuanzia:
(1) Jambo la kwanza linahusiana na jinsi mtindo wa kifedha wa Wikimedia unavyoendeleza dhamira yetu. Makadirio ya siku zijazo yanaonyesha kwamba, kwa sababu mbalimbali, uchangishaji wa pesa mtandaoni na kupitia mabango huenda usiendelee kukua kwa kiwango sawa na miaka iliyopita. Tuna mipango kadhaa ya muda mrefu inayoendelea ili kusaidia kupunguza hatari hii na pia kubadilisha njia zetu za mapato.
- Sasisho lilichapishwa hivi karibuni kuhusu jukumu muhimu la Waraka wa Wikimedia katika kukuza usaidizi wa muda mrefu kwa miradi.
- Sambamba na hilo, tunaendelea kutathmini uwezo wa Wikimedia Enterprise wa kuboresha hali ya matumizi ya wasomaji zaidi ya tovuti zetu huku tukiwa na makampuni mengi yanayotumia maudhui yetu ili yaweze kusaidia harakati zetu.
- Kwa upande wa matumizi, tumekabiliana kwa kupunguza kasi ya ukuaji wa Shirika lenyewe, huku tukiongeza rasilimali za kifedha zinazosaidia sekta zingine za harakati.
Tunahitaji mtindo wa muda mrefu wa kifedha unaolingana na matarajio yetu na rasilimali zetu ili kutekeleza mipango kwa ufanisi.
(2) Jambo la pili ni vipaumbele vyetu vya bidhaa na teknolojia, ambavyo mwaka huu vinazingatia mahitaji ya teknolojia ya wachangiaji wa Wikimedia (kutoka kwa wale walio na haki zilizopanuliwa, kwa wageni, hadi washirika wa kitaasisi kama mashirika ya GLAM). Hii inaanzia:
- malengo ya jumla yaliyoainishwa katika mpango wa sasa wa kila mwaka, ambao uliamuliwa kufuatia kipindi cha mapitio ya jumuiya, pamoja na maoni yaliyotolewa na wajitoleaji moja kwa moja kwa Afisa Mkuu mpya wa Shirika wa Bidhaa na Teknolojia, Selena Deckelmann.
- Kuendeleza vipaumbele muhimu vilivyotolewa na wahariri walio na haki zilizopanuliwa. Hili limeungwa mkono na uboreshaji wa programu ya Udhibiti wa Kurasa Mpya, kwa kutengeneza mtiririko wa kazi katika programu ya Android ya kufuatilia mahariri, kwa kuunda mfumo unaowaongoza wachangiaji wapya kufanya hariri zenye marejeo mazuri, na kwa kukuza uwezo wa kila jumuiya kusanidi vipengele ili kujitosheleza mahitaji yao wenyewe.
- Usaidizi ulioongezeka kwa Wikimedia Commons uliojumuisha masasisho hadi Thumbor, usaidizi wa OpenRefine, na kazi nyingine. Pia kuhamia toleo jipya zaidi la leseni ya Creative Commons kwenye Wikipedia, kwa kujibu maombi ya toleo linalosomeka zaidi na binadamu na la kimataifa la leseni ya bure ya utamaduni inayotumiwa kwenye Wikipedia ili kufanya maarifa yapatikane bila malipo.
- Kujitolea kukagua na kuboresha mchakato wa orodha ya matamanio ya jumuiya ili kushughulikia vyema mahitaji ya watumiaji mbalimbali, matatizo ya kiufundi yanayoongezeka, na ushirikiano wa kina kati ya timu za Shirika za Bidhaa na Teknolojia na wafanyakazi wa kujitolea wa kiufundi. Matokeo ya utafiti wa orodha ya matamanio ya 2022 na 2023 yanaonyesha jinsi tunavyoleta pamoja ujuzi na utaalamu unaofaa zaidi kwa maombi. Kwa mfano, wakati timu ya Comm-Tech iliwasilisha Ushughulikiaji bora diff kwaajili ya kutenganisha aya - seti ya vipengele vya kurudia ili kuboresha utumiaji wa msingi wa uhariri, mojawapo ya vipengele vinavyotafutwa sana - hali nyeusi kwa usomaji - sasa inachukuliwa na timu ya Wavuti. Tutaendelea na ushirikiano zaidi ili kujenga mfumo wa kujibu maombi ya matakwa ya kiufundi unaobadilika na ulioendelevu.
- Kuendana na kuongezeka kwa majukumu ya udhibiti na kisheria katika jukumu letu kama mwenyeji wa kiufundi wa miradi ya Wikimedia, ambayo inajumuisha mahitaji ya ziada ya Sheria ya Huduma za Kidijitali inayoainisha Wikipedia kama Jukwaa Kubwa Sana la Mtandao (VLOP) na kujibu kanuni nyingine zinazokuja ku kutetea modeli ya kipekee ya Wikipedia ya kujitawala kwa jamii.
- Kuendeleza mazungumzo ya jumuiya kuhusu akili bandia inayoendelea kuzalishwa, huku pia tukiboresha miundombinu yetu ya mashine kujifunza ya kisasa ili kusaidia utumiaji wa zana za ML zilizopangiliwa kwenye miradi yetu. Hii imejumuisha kujaribu iwapo na jinsi tunavyoweza kutoa maarifa ya kuaminika, yanayothibitishwa kupitia mfumo wa nje ya jukwaa visaidizi vya AI kama vile ChatGPT. Tumefanya majaribio pia kuhusiana na namna gani mashine kujifunza kunaweza kutumiwa kusaidia jumuiya ndogo za wiki kudhibiti kiotomatiki mabadiliko yanayoingia.
- Lugha ambazo hazijatumika vyema na tafsiri za mashine huria kupitia huduma mpya ya utafsiri – MinT – inayotumika kwa zaidi ya lugha 200, zikiwemo lugha 44 ambazo kwa mara ya kwanza zina tafsiri ya mashine.
- Kuweka rasilimali zaidi kwa matengenezo na usaidizi wa programu ya MediaWiki huku tukianza kufikiria pamoja kuhusu mpango wa baadaye.
- Kama sehemu ya kujitolea kwetu kwaajili ya usawa wa maarifa, tumeongeza kituo kipya cha kutunza kache huko Amerika Kusini ili kuongeza mwitikio wa tovuti katika eneo hili.
- Kupanua uwezo wa waandaaji wa kampeni na hafla kwa kuboresha uwezo wa Usajili wa Tukio na kuanza kutumia njia za waandaaji kutangaza kuhusu kampeni zao.
- Tunawaletea wasomaji maboresho kama vile uwezo wa kupangilia uzoefu wao wa kusoma kupitia hali nyeusi na udhibiti wa ukubwa wa maandishi.
- Kujaribu kuhusiana na jinsi tunavyoweza kushirikisha maarifa bila malipo na vijana wa kimataifa na kuwaalika katika miradi yetu kwenye programu za media wasilianifu ambako wanapenda kutumia muda wao (k.m., TikTok, Instagram Reels).
- Kuweka kipaumbele kwenye vipengele vya usalama kuanzia na matoleo ya kwanza kabisa ya Mfumo wa Kuripoti Matukio, ili wahariri waweze kuripoti unyanyasaji kwa njia ya angavu, kuanzisha mfumo wa utekelezaji unaoendeshwa na jumuiya kwa ajili ya Mwongozo wa Kanuni za Maadili wa Kimataifa ili kuongeza usalama na ujumuishaji kwa washiriki katika miradi yote ya Wikimedia.
(3) Hatimaye, tunatathmini kanuni za kufafanua majukumu na wajibu mkuu wa Shirika. Kama harakati ambazo zimejengwa juu ya nguvu ya kutafuta watu wengi, ni mgawanyiko gani bora wa kazi tunaohitaji ili kufikia malengo yetu? Hii inakusudiwa kusaidia mijadala ya katiba ya harakati, na pia kutambua moja kwa moja changamoto katika miundo yetu ya kufanya maamuzi na utawala:
- Je, lengo la kuunda sekta za ziada litakuwa nini sasa, na je, tunaweza kubadilisha au kufunga sekta nyingine ili kufikia malengo haya?
- Je, kuna majukumu ambayo Shirika linapaswa kuacha kuyashughulikia au kuruhusu wengine kuongoza?
- Je, tunawezaje kuharakisha vipi ufanyaji maamuzi ya kiufundi?
- Je, tunahakikisha vipi kwamba wachangiaji wa kimataifa, wawe wamepangwa katika miundo shirikishi au la, wanaweza kutoa maoni na mahitaji yao kwa ufanisi na kwa namna ya kufaa?
- Ni wapi na jinsi gani tunapaswa kuendelea kutathmini, kurudia, na kukabiliana na mahitaji yanayobadilika ya harakati zetu na ulimwengu unaotuzunguka?
Kwa kweli hii sio orodha kamili ya maswala yote ambayo yanahitaji kushughulikiwa. Ni sehemu ya kuanzia kwa mada muhimu ambayo naamini yanahitaji maono ya mbali zaidi. Utaona katika sehemu inayofuata kwamba naomba msaada wako katika kufahamu jinsi tunavyoendelea kutoka hapa.
Mwaaliko wa Mazungumzo: 2024...
Pamoja na kujifunza kuhusu kazi za Wikimedia katika miaka hii miwili iliyopita, pia nimeelekeza nguvu zangu nyingi katika kujifunza kuhusu njia zetu za kufanya kazi pamoja. Kutimiza dhamira yetu kunahitaji mwingiliano zaidi wa wanadamu, ndani na nje ya wiki, ambao umeundwa ili kuunda uelewaji zaidi wa pamoja, na tunatumai kukuza uaminifu. Kurejeshwa kwa mikusanyiko ya ana kwa ana kumekuwa muhimu kwa kikundi kidogo cha wafanyakazi wetu wa kujitolea, kutoa nafasi kwa ajili ya kukutana upya, kujichaji upya na kushughulikia masuala magumu pamoja katika chumba kimoja. Uongozi wa Shirika pia umekuwa ukifanya kazi kwa bidii zaidi kushirikisha habari za shirika na kuwa na mazungumzo ya kibinafsi kwenye Wiki na katika majukwaa mengine ya kidijitali.
Lengo ni kuweka juhudi zaidi na makusudi katika kupashana habari zilizo sahihi, kwa wakati ufaao, na kwa njia ifaayo, hata kama tunajua kwamba hatuwezi kamwe kufikia matarajio ya kila mtu.
Pia ni muhimu kwetu kwa mwaka mzima - rasmi na kikawaida. Ili kuunga mkono hili, katika miezi michache ijayo ninawaomba Wadhamini wetu na wenzangu katika Shirika la Wikimedia Foundation kuungana nami katika aina tofauti ya ziara ya kusikiliza: zaidi ya mazungumzo ya pande mbili ambayo yameundwa kusikiliza kwa umakini kile kilichopo akilini mwako kwa sasa, na pia kushirikisha maendeleo na mawazo kuhusu mpango wetu wa miaka mingi.
Tunaweza kutumia muda kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu katika muktadha wa:
- matukio muhimu yanayotokea mwaka wa 2024 (k.m., uchaguzi muhimu, katiba ya harakati, utekelezaji wa Mwongozo wa Kimataifa wa Maadili na Nidhamu, mahitaji ya kufuata Sheria ya Huduma za Kidijitali, na jinsi ya kuwajibu wabunge kote ulimwenguni wanaohusika na athari za teknolojia za kidijitali kwenye jamii);
- mpango wetu wa kila mwaka unaounga mkono malengo ya mkakati wa 2030 wa usawa wa maarifa na maarifa kama huduma;
- maswali ya muda mrefu zaidi yanayohusu kulinda miradi yetu kwaajili ya vizazi vijavyo;
- na kitu kingine chochote kwenye akili yako!
Natumai utaamua kushiriki. Unaweza kuchagua kujiandikisha kwenye wiki au nje ya wiki kati ya Oktoba na Februari, ikijumuisha mazungumzo ya kibinafsi na Wadhamini, na mimi mwenyewe na viongozi wengine wa Shirika. Mazungumzo haya yanakusudiwa kuboresha mijadala katika mkutano wa mipango ya kimkakati ya Bodi hapo ifikapo mwezi Machi, na muhtasari wa kile tulichosikia kitashirikishwa kwa kila mtu kabla ya Machi.
Tunu ya Shirika la Wikimedia ya kusikiliza na kushirikisha kwa dhamira zaidi itatoa mwelekeo wa jinsi tunavyojitokeza, na ninatumai kila mtu ambaye ana nia ya kushiriki ataleta mbinu zinazofanania na jambo hili.
Kama ilivyo kawaida, ninakaribisha maoni yako kwenye ukurasa wa majadiliano au kunitumia barua pepe moja kwa moja kwenye miskander@wikimedia.org.
Maryana
Maryana Iskander
Mkurugenzi Mtandaji(CEO) wa Wikimedia Foundation
Wanawikimedia ambao wameonesha nia
Talking:2024 Statistics
Between October 2023 and Oktoba 2024, we have contacted 218 Wikimedians and managed to connect with 158.
These conversations have stretched across all regions of the world. We have learned from prolific community members to recent newcomers, from technical volunteers to stewards, event organizers, and affiliate leaders. Since these discussions were intended to improve deliberations at the Board’s strategic planning retreat in early March, here is a summary of some of the feedback we've heard so far!
Regional breakdown
Region | Percentage |
---|---|
Africa | 13% |
CEE & CA | 17% |
ESEAP | 12% |
Latin America & the Caribbean | 10% |
Middle East & North Africa | 6% |
North America | 17% |
North and Western Europe | 20% |
South Asia | 5% |
Who did we speak to?
- 25% were follow-ups to the original listening tour
- 50% were new suggestions by Movement Communications and other colleagues
- 25% signed up on wiki.
We would love to add your voice to all the helpful feedback we have already received — we are listening (on-wiki, in 1:1 conversations, in small groups, in person), and what we hear will impact the Foundation's long-term plans. Please consider joining a conversation soon.