Jump to content

Chaguzi za Wikimedia Foundation/2022/Miongozo ya ustahiki wa mpigakura

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation elections/2022/Voter eligibility guidelines and the translation is 87% complete.
Outdated translations are marked like this.

Ustahiki wa kupiga kura

Kanuni ya jumla

Ili ustahili kupiga kura ni lazima usiwe umezuiwa kwenye zaidi ya mradi mmoja.

Wahariri

Unaweza kupiga kura kwa kutumia akaunti yoyote iliyosajiliwa unayomiliki kwenye Wikimedia wiki. Unaweza kupiga kura mara moja tu, bila kujali unamiliki akaunti ngapi. Ili kustahiki, akaunti hii moja lazima:

  • isiwe imezuiliwa kwenye zaidi ya mradi mmoja;
  • isiwe ni bot;
  • na uwe umefanya angalau hariri 300 kabla ya tarehe 5 Julai 2022 katika mradi wowote wa Wikimedia;
  • na uwe umefanya angalau mabadiliko 20 kati ya tarehe 5 Januari 2022 na 5 Julai 2022.

AccountEgibility tool inaweza kutumika kuthibitisha kwa haraka vitu vya msingi vya ustahiki kwa mhariri kupiga kura.

Watengeneza programu

Watengenezaji wa programu wanaruhusiwa kupiga kura ikiwa:

  • ni wasimamizi wa seva za Wikimedia wenye haki ya ufikiaji wa Sheli
  • au wamefanya majitoleo ya pamoja angalau mara moja kwenye repos zozote za Wikimedia kwenye Gerrit, kati ya 5 Januari 2022 na 5 Julai 2022.

Vigezo vya ziada

  • au wamefanya majitoleo angalau mara moja kwenye repo yoyote katika nonwmf-extensions au nonwmf-skins, kati ya 5 Januari 2022 na 5 Julai 2022.
  • wamefanya majitoleo ya pamoja angalau mara moja kwenye repo yoyote ya zana za Wikimedia (kwa mfano magnustools) kati ya tarehe 5 Januari 2022 na 5 Julai 2022.
  • au wamefanya angalau mabadiliko 300 kabla ya tarehe 5 Julai 2022, na mabadiliko 20 kati ya 5 Januari 2022 na 5 Julai 2022, kwenye Translatewiki.
  • au watunzaji/wachangiaji wa zana zozote, bot, hati za watumiaji, vifaa, na moduli za Lua kwenye Wikimedia wiki.
  • au wamejihusisha kwa kiasi kikubwa katika kubuni na/au kukagua michakato ya maendeleo ya kiufundi inayohusiana na Wikimedia.

Kumbuka: Ikiwa unakidhi vigezo vikuu, utaweza kupiga kura mapema. Kwa sababu ya vikwazo vya kiufundi vya SecurePoll, watu wanaohitajika kuwa na vigezo vya ziada huenda wasiweze kupiga kura moja kwa moja, isipokuwa hadi watimize vigezo hivyo vya ziada. Iwapo unaona kuwa unakidhi vigezo vya ziada, tafadhali tuma barua pepe kwa board-elections@lists.wikimedia.org yenye hoja zako angalau siku nne kabla ya tarehe ya mwisho ya kupiga kura, yaani, tarehe 30 Agosti 2022 au kabla yake. Ukitimiza vigezo, tutakuongeza kwenye orodha tofauti, ili kuweza kupiga kura.

Wikimedia Foundation staff and contractors

Current Wikimedia Foundation staff and contractors qualify to vote if they have been employed by the Foundation as of 5 July 2022.

Wikimedia movement affiliates’ staff and contractors

  • Chapta za sasa za Wikimedia, Shirika la Mada au wafanyakazi wa kikundi cha watumiaji na wanakandarasi wanaruhusiwa kupiga kura ikiwa wameajiriwa na shirika lao kuanzia tarehe 5 Julai 2022.
  • Wanachama wa mashirika rasmi kama inavyofafanuliwa katika sheria ndogo za Chapta za sasa za Wikimedia, Mashirika ya Mada au vikundi vya watumiaji wanaruhusiwa kupiga kura ikiwa wamekuwa wakihudumu katika shughuli hizo kuanzia tarehe 5 Julai 2022.

Kamati ya Ushirikiano na Kamati ya Uchaguzi itathibitisha orodha ya Washirika wa Wikimedia wanaoruhusiwa kufikia tarehe 1 Agosti 2022.

Wajumbe wa bodi ya Wikimedia Foundation na wajumbe wa bodi ya Ushauri

Wanachama wa sasa na wa zamani wa Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia Foundation na Bodi ya Ushauri ya Wikimedia Foundation.

Wajumbe wa Kamati ya Harakati za Wikimedia

Wanachama wa sasa wa Kamati ya Harakati za Wikimedia wanaruhusiwa kupiga kura ikiwa wamekuwa wakihudumu katika majukumu hayo kuanzia tarehe 5 Julai 2022.

Kamati ya Uchaguzi itatangaza orodha ya Kamati za Harakati za Wikimedia zinazoruhusiwa kuoiga kura kufikia tarehe 1 Agosti 2022.

Waandaaji wa jumuiya ya Wikimedia Movement

Waratibu wa jumuiya walio na hadhi nzuri, ambao hawana sifa ya kupiga kura chini ya kategoria nyingine, waruhusiwa kupiga kura iwapo watakuwa na moja wapo ya yafuatayo:

  • wametuma maombi, kupokea na kuripoti angalau ruzuku moja ya Wikimedia Foundation tangu tarehe 1 Septemba 2021.
  • walikuwa waratibu wa angalau tukio moja la hackathon lililofadhiliwa, shindano au tukio lingine la Wikimedia lililo na makala kwenye-wiki na angalau wahudhuriaji/wageni/washiriki 10 kati ya tarehe 5 Januari 2022 na 5 Julai 2022.

Vigezo vya ziada

Iwapo unaona kuwa unakidhi vigezo vya ziada, tafadhali tuma barua pepe kwenda board-elections@wikimedia.org na hoja hizo angalau siku nne kabla ya tarehe ya mwisho ya kupiga kura, yaani, tarehe 30 Agosti 2022 au kabla yake. Ukitimiza vigezo, tutakuongeza kwenye orodha tofauti, ili kuweza kupiga kura.