Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Mapitio ya Rasimu/Ujumbe wa Mwaliko
Mwaliko wa kushiriki katika Mazungumzo
HelloSamahani kwa kuchapisha ujumbe huu hapa,na pia endapo unasoma ujumbe huu kwa lugha isiyo yako (usiyoizoea).Tafsiri za tangazo lifuatalo zinaweza kupatikana kwenye Ukurasa wa meta. Please help translate to your language. Thank you!
Habarini nyote. Tunayo furaha isiyo na kifani kuwashirikisheni Rasimu ya Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Nidhamu (Universal Code of Conduct) ambao Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia Foundation iliridhia uundwe mwanzoni mwa mwaka huu, kwaajili ya kuupitia na kutoa maoni yako. Mjadala utakuwa wazi mpaka Octoba 6, 2020.
Kamati ya uundaji wa mwongozo huo inapenda kujifunza ni sehemu zipi za rasimu hiyo zinaweza kuleta changamoto kwako binafsi au kwenye kazi yako.Kitu gani unadhani kinakosekana katika rasimu hii? Kipi unapenda juu ya mwongozo huu, na kipi unadhani kinatakiwa kuboreshwa?
Tafadhali jiunge katika majadiliano na jisikie huru kualika wengine pia watakaopenda kushiriki katika mazungumzo hayo.
Ili kupunguza vizingiti vya lugha, unakaribishwa kutafsiri ujumbe huu na Rasimu ya UCoC. Pia wewe na jumuiya yako mnawezkuchagua kutoa maoni yenu/mrejesho kwa kutumia lugha zenu za asili.
Ili kujifunza zaidi kuhusiana na mradi wa UCOC, angalia ukurasa wa Mwongozo wa UCoC katika meta na pia angalia Maswali yaulizwayo mara kwa mara kuhusu UCoC
Tunatanguliza shukrani za pekee kwa ushiriki na mchango wako, ni sisi The Trust and Safety team at Wikimedia Foundation