Matukio ya Kampeni
Kiendelezi cha Tukio la Kampeni ni zana madhubuti iliyoundwa ili kuboresha usimamizi na mwonekano/ugunduzi wa matukio ndani ya harakati za Wikimedia. Kiendelezi hiki kinatmbulisha mkusanyiko wa vipengele vinavyolenga kufanya mpangilio na ushiriki wa tukio kuwa rahisi na bora.
Kiendelezi cha CampaignEvent kinakuja na vipengele muhimu kadhaa:
Zana ya Usajili wa Tukio
Zana ya Usajili wa Tukio huruhusu waandaaji wa kampeni kudhibiti usajili wa tukio moja kwa moja kwenye wiki. Zana hii hurahisisha mchakato wa kufuatilia waliohudhuria, kudhibiti maelezo ya usajili, kutuma barua pepe kwa washiriki waliosajiliwa, mwingiliano na dashibodi ya Mipango na Matukio na mengine mengi.
Orodha ya Ushirikiano
Orodha ya Ushirikiano ni orodha ya kimataifa ya matukio yote yanayotumia Usajili wa Matukio na orodha ya WikiProjects zote kwenye miradi ya wiki mahalia, hivyo kurahisisha watu kupata fursa za kushirikiana na kuunganishwa na wachangiaji wengine kwenye wiki.
Orodha ya Mialiko
Orodha ya Mialiko ni zana iliyoundwa kusaidia waandaaji kutambua watumiaji ambao wanaweza kutaka kujiunga na miradi au hafla zao. Inafanya kazi kwa kuangalia orodha ya vifungu ambavyo mratibu anapanga kuzingatia wakati wa shughuli, na kisha kupata watumiaji wa kualika kulingana na vigezo vifuatavyoː baiti walizochangia kwenye makala, idadi ya mabadiliko waliyofanya kwenye makala zao, hesabu ya jumla ya uhariri kwenye wiki, na jinsi ambavyo wamehariri kwenye miradi ya wiki hivi karibuni.
Maboresho ya Baadaye
Kiendelezi cha CampaignEvent kimeundwa kwa kuzingatia unyumbufu, kikiruhusu kuunganishwa kwa zana za ziada ili kusaidia waandaaji na washiriki wa kampeni. Zana moja kama hiyo inayoundwa kwa sasa ni Orodha za Mialiko. Zana hii itasaidia waandaaji kwa kupendekeza washiriki watarajiwa ambao wanaweza kupendezwa na matukio yao yajayo, kuboresha zaidi ushiriki na mahudhurio.